KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 1, 2016

JPM AMPANDISHA CHEO ASKARI ALIYETUKANWA NA MKE WA WAZIRI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernesti Mangu kumpandisha cheo askari wa Usalama barabarani ambaye alitukanwa na Mke wa Waziri wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi. Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa. Aidha Rais Dr. Magufuli amesema ameshamuonya Waziri huo ambaye mke wake amemtukana askari wa Usalama Barabarani. Wakati akitoa agizo hilo, rais amesema hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko juu ya sheria.

No comments:

Post a Comment