| Msanii
wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kupitia mwanasheria wake Aman G.
Tenga kutoka Law Associates (Advocate) ameandika barua ya kumtaka
mtangazaji maarufu wa Clouds Fm, Gardner G. Habash, kuomba msamaha mbele
ya umma kutokana na kauli yake ya uzalilishaji aliyoitoa dhidi yake.
Gardner
ambaye alikuwa mume wa muimbaji huyo wa Ndindindi, anatuhumiwa
kulifanya kosa hilo mnamo tarehe 6 May 2016, akiwa kama mshereheshaji
tamasha la Miss TIA 2016 lililofanyika CDS Park (zamani TCC) ambapo
alidaiwa kutamka kwa makusudi maneno ya udhalilishaji na kejeli “Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi” mbele ya umma.
Baada ya wiki moja toka tukio hilo litokea, Lady Jaydee kupitia mwanasheria wake ameandika barua hii.
|
No comments:
Post a Comment