Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016. |
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho akielezea umuhimu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 katika mkutano wa wadau wa utafiti huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016. |
Mkurugenzi Mkazi wa ICAP Tanzania Dkt. Fernando Morales akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016. |
Baadhi ya
washiriki waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
(hayupo pichani) katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti huo uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi
Agosti, 2016. (PICHA NA EMMANUEL GHULA).
……………………………………………………………………………………….
Na Veronica Kazimoto
Wito umetolewa kwa wadau pamoja na wananchi ili kushiriki kikamilifu katika kuwezesha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
Akizungumza katika Mkutano wa
Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka
2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema wananchi kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wana mchango mkubwa katika kufanikisha
upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
“Leo hii tumekutana na wadau
mbalimbali wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa
mwaka 2016/2017 utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya
kujadili na kushauriana namna ya kufanya utafiti huu kwa ufanisi ili
kupata takwimu bora zitakazosaidia katika kutunga sera na kupanga
mipango ya maendeleo nchini”, amesema Dkt. Chuwa.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa
utafiti huu unategemea sana ushiriki wa wananchi kwani wao ndio wadau na
wahusika wakuu ambao wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha ili
kurahisisha upatikanaji wa takwimu rasmi zitakazosaidia Taifa katika
kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya watanzania wote.
Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya
Taifa ya Takwimu ipo katika harakati za kukamilisha maandalizi ya
utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania 2016/2017 ambao
utaanza kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Aidha Dkt. Chuwa amesema
utafiti huu ni wa kipekee ukilinganishwa na tafiti zilizotangulia
kutokana na kuongezeka kwa viashiria vitakavyo chunguzwa ikiwemo
kuangalia kiwango cha CD4, kiwango cha maambukizi mpya, upatiakanaji wa
huduma zinazohusiana na UKIMWI pamoja na kupima watoto wadogo wenye umri
chini ya mwaka mmoja.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa
utafiti huu kutasaidia Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini
hasa katika kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI na namna ya
kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkazi wa ICAP nchini, Dkt. Fernando Morales amesema utafiti huu ni wa
muhimu katika kupima viashiria na matokeo ya UKIMWI kwa nchi ambazo
zimekuwa zikipata msaada wa kupambana na UKIMWI kutoka Serikali ya
Marekani.
“Lengo la Utafiti huu ni kupata
viashiria ambavyo vinasababisha maambukizi mapya pamoja na kupima jinsi
gani Taifa limeweza kupambana na ugonjwa wa UKIMWI nchini”, amesema
Dkt. Morales.
Utafiti wa Viashiria na Matokeo
ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 unafanyika katika nchi Ishirini
(20) Afrika ambapo kwa sasa nchi nane (8) zinaendelea na utafiti huu
zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Malawi, , Lesotho, Swaziland, Uganda, Namibia
na Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment