KINSHASA,
CONGO: Mwili wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Papa
Wemba, ambao upo ndani ya Nchi hiyo unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao
keshokutwa siku ya Jumatano ya Mei 4. 2016 tofauti na taarifa ya awali
iliyoeleza kuwa nguli huyo angezikwa jioni ya Mei 3.
Modewjiblog
kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka katika vyanzo vya habari
ikiwemo kurasa wa mtandao wa mwanamuziki huyo, ilitoa taarifa fupi ya
ratiba ya maziko hayo na taratibu za kuaga mwili huo.
Leo siku ya Jumatatu Mei 2
- Kuanzia saa mbili asubuhi mwili utatolewa Hospitali na kuzungushwa katika mitaa ya nchi hiyo na kuelekea katika eneo maalum la kuagia.
- Kuanzia saa saa nne asubuhi hadi mchana Rais wa DR Congo, Joseph Kabila ataongoza wananchi wa Congo na wanamuziki kuaga mwili wa Papa na kisha jioni mwilI huo utapelekwa kijijini kwa nguli huyo katika kijiji cha Molokai na utalala kijijini kwake.
- Mei 4.2016 maziko
- Kwa ratiba hiyo inaonyesha baada ya mwili huo kulala kwa siku moja katika kijiji cha Papa Wemba na kuendelea na sara na mambo ya mila na kufuatia maziko
- Papa Wemba alifariki hivi karibuni jijini Abidjan nchini Ivory Coast ambapo awali alipoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.
- NB: Modewjiblog itaendelea kukuletea kila kinachoendelea na endapo ratiba itabadilika tutawajuza pia,..
Pichani ni enzi za uhai wake mwanamuziki Papa Wemba
Pichani
enzi za uhai wake: Mwanamuziki Papa Wemba alipokuja Tanzania, kwenye
tamasha la Karibu Music Festival 2015, Bagamoyo-Pwani. Picha na Andrew
Chale-Modewjiblog-Bagamoyo).
Mwanamuziki
Papa Wemba (kushoto) enzi za Uhai wake akipata picha ya ukumbusho na
Mwandishi Mwandamizi wa mtandao huu wa Modewjiblog, Andrew Chale wakati
wa mahojiano maalum kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015,
Bagamoyo Pwani. - Mtandao wa MODEWJIBLOG, unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wafuasi wote wa mwanamuziki Papa Wemba kwa kuondokewa na kipenzi chao.Nasi tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu hivyo tunatoa pole.


No comments:
Post a Comment