KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 10, 2016

PSPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSOMEA KWA WANAFUNZI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI MWANZA NA GEITA

Afisa Uendashaji wa PSPF Mkoa wa Geita, Bw. Noel
Tuga, akiwapa maelezo wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya
msingi Nyansalwa namna ya kutumia vifaa vilivyopo kwenye mabegi PSPF iliyotoa
msaada. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi
Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.

Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta
Mnyamani ,akiongea na kamati ya shule ya Msingi Igaka (ambao hawapo pichani)
pamoja na wanafunzi kuhusiana na lengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kusaidia
jamii hasa kwenye nyanja ya elimu nchini.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia
msaada uliotolewa na PSPF kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu shuleni
hapo.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka,
Bw. Jumanne Masumbuko, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake
kwa masaada wa mabegi ya shule yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni
wa PSPF.
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mwanza,
Bw. Salim Salum, akitoa rai kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka iliyopo
Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kusoma kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu
na kuja kulitumikia Taifa katika siku za baadaye.

No comments:

Post a Comment