![]() |
Na Veronica Simba-Maelezo
Serikali
imesema ushindani kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya
nishati, ndiyo njia bora zaidi itakayowezesha kuwapata wawekezaji wenye
vigezo vinavyotakiwa.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyasema hayo jana, Mei
10, alipokutana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio
Shoji na Ujumbe wake, ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika
uzalishaji na usafirishaji wa umeme nchini, kwa kutumia vyanzo
mbalimbali ikiwemo gesi asilia na jua.
“Kampuni
nyingi zimeonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati. Serikali
inao uhitaji mkubwa wa wawekezaji walio makini, hivyo tunahitaji
kuwapata wawekezaji wenye vigezo kwa kutumia ushindani unaozingatia
uwazi,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Aliongeza
kuwa, ili kuwarahisishia wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta
ya nishati nchini, Wizara inaandaa taarifa maalum itakayobainisha maeneo
yanayohitaji uwekezaji pamoja na vipaumbele vyake.
Alisema,
taarifa hiyo itakuwa tayari na kutolewa mwishoni mwa mwezi huu (Mei 31,
2016) na kwamba itasambazwa kwa wadau wote wa ndani na nje ya nchi
kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ikiwamo tovuti ya wizara.
Profesa
Muhongo alieleza kuwa, taarifa hiyo pamoja na mambo mengine, itawapa
fursa wawekezaji wenye nia, kuchagua aina ya uwekezaji wanaohitaji
kufanya na katika maeneo ambayo wanadhani watakuwa na uwezo wa kumudu
ushindani kutoka kwa wawekezaji wenzao kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Akifafanua
zaidi, Profesa Muhongo alisema kuwa, zoezi la kuwashindanisha
wawekezaji walioonesha nia, litakuwa ni endelevu na litakuwa likifanyika
kila baada ya muda fulani, ambao utabainishwa katika taarifa husika
inayotarajiwa kutolewa.
Akitoa
mfano, alisema kuwa, siyo lazima kumpata mwekezaji katika zoezi la
ushindanishaji, hivyo ni muhimu zoezi liwe endelevu ili kuweza kutoa
fursa kwa wawekezaji wengi zaidi kushiriki na hivyo kumpata mwekezaji
mwenye vigezo vyote ambavyo Serikali inavihitaji.
“Endapo
tutaendesha zoezi la ushindanishaji wawekezaji na wote
walioshindanishwa wasipotimiza vigezo vinavyotakiwa, hatulazimiki
kumchukua yeyote tu. Tutakachofanya ni kutokumchukua yeyote kati yao na
hivyo kuendelea na zoezi hilo baada ya muda tutakaoubainisha, hadi pale
tutakapowapata wawekezaji wenye vigezo tunavyovitaka.”
Profesa
Muhongo alibainisha kuwa, mchanganyiko wa nishati ambao Serikali
imekusudia kuutumia kama vyanzo vya kuzalisha umeme nchini kwa sasa ni
pamoja na gesi asilia, maji, upepo, jua, makaa ya mawe, mvuke (maji
moto) na tungamotaka.
|
![]() |
| Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo (Kulia), akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji, baada ya kikao baina ya Wizara ya Nishati wa Nishati na Madini na Kampuni husika, kilichofanyika Mei 10 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. |
| Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Katikati), akiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Kampuni ya KOYO ya Japan katika kikao kilichofanyika Mei 10 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. |




No comments:
Post a Comment