![]() |
| Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
…………………………………………
SERIKALI imekanusha taarifa
kuhusiana na zuio la mashine za kukoboa mpunga na mahindi katika
Halmashauri ya Mji wa Kahama kwamba zisifanye kazi wakati wa usiku au
saa 24.
Kauli hiyo imetolewa
leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum, Mhe. Salome Makamba aliyetaka kujua utayari wa Serikali
wa kuruhusu viwanda Wilaya ya Kahama kufanya kazi masaa 24 ili kufidia
uzalishaji uliokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokatika nyakati za
mchana.
Mhe. Jafo amesema
kuwa, Serikali haijota zuio lolote kwa mashine katika Halmshauri hizo na
amefafanua kuwa changamoto iliyopo ni kwamba viwanda hivyo vimekuwa
vikitumia umeme wa jenereta ambao hautoshelezi kuendesha mashine wakati
wote, hivyo kupelekea kuwepo na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa
mara.
Amefafanua kuwa,
Halmshauri imewasiliana na Meneja wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania
(TANESCO) Kahama na tayari tatizo hilo limeanza kushughulikia ili kupata
umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa ambapo tayari kituo cha
usamabazaji kimeanza kujengwa Kahama.
Ameongeza kuwa
Halmashauri inahamasisha wawekezaji wa viwanda vidogo vya kukoboa
mpunga, mahindi na mazao mengine ili kupanua wigo wa mapato kupitia
ushuru wa huduma (Service Levy) na ajira kwa vijana.
“Hakuna sababu yoyote
kwa Serikali kuzuia wawekezaji katika viwanda vidogo na vikubwa, azma ya
Serikali ni kupanua uwekezaji wa viwanda kadri iwezekenavyo kwa
kuzingatia fursa zilizopo, tunachofanya ni kuboresha mazingira
yatakayosaidia uwekezaji huo kufanyika kwa faida ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa umeme wa uhakika unakuwepo.
|
May 17, 2016
SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU ZUIO LA MASHINE ZA KUKOBOA NAFAKA HALMASHAURI YA KAHAMA KUFANYA KAFANYA KAZI SAA 24
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment