![]() |
Waziri
wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo ameliambia Bunge Mjini
Dodoma kwamba miradi ya umeme vijijini (REA) haijaathirika chochote kwa
Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) kuondoa misada yake
Tanzania.
Muhongo
ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji Peter Msigwa aliyetaka kujua serikali imepata hasara kiasi
gani kwa MCC kuondoa fedha zake katika miradi ya umeme nchini.
Akijibu
swali hilo Prof Muhongo amesema fedha za MCC zilikuwa haziendi kwenye
miradi ya maendeleo ya umeme vijijini hivyo miradi hiyo itaendelea kama
ilivyopangwa.
''Hakuna
dola hata moja ya MCC iliyokuwa inaenda kwenye umeme vijijini fedha
zilikuwa zikienda kwenye miradi ya maji, barabara na nishati lakini siyo
umeme wa vijijini na fedha za kwenye nishati zilikuwa hazivuki theluthi
moja hivyo kama umejiandaa kulima hekari 8 akakuongezea mtu 2 ili
zifike 10 siku akiondoa za kwake utandelea na zako 8 kama kawaida''- Amesisitiza Prof. Muhongo.
Bodi
ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilisema Tanzania haijatimiza
viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika
hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa
jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za
Tanzania.
Kwa
awamu ya kwanza Tanzania ilipokea Dola 698 milioni na moja kati ya
mambo yaliyosababisha MCC kuondoa fedha zao ni pamoja na kurudiwa kwa
uchaguzi wa Zanzibar.
|
May 16, 2016
SERIKALI YASEMA KUSITISHWA KWA BAADHI YA MISAADA YA WAHISANI HAKUJAATHIRI SEKTA YA NISHATI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment