![]() |
| Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
…………………………………….
SERIKALI imetenga Shilingi bilioni
59.5 katika Bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi
vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa.
Taarifa hiyo imetolewa
leo Bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Dkt. Abdallah Possi (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti
Maalum, Mhe. Esther Mahawe aliyetaka kujua ni lini fedha zingetolewa na
Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya
njia bora ya kutumia fedha hizo.
Dkt. Possi amesema
kuwa, fedha hizo zitatolewa mara baada ya kuidhinishwa na Bunge hilo na
baada ya kukamilisha taratibu mahususi zinazolenga kuhakikisha uwepo wa
tija katika matumizi ya fedha hizo.
Ameongeza kuwa, kuhusu
mpango bora wa Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi, Serikali inaendelea
kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji wa fedha hizo ikiwa
ni pamoja na utoaji wa elimu ya Ujasiriamali.
“Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI
imepewa kazi ya kuratibu utekelezaji wa mpango huo”, alisema Dkt.
Possi.
|
May 10, 2016
SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 59.5 KWA AJILI YA KUWAWEZESHA WANANCHI VIJIJINI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment