Mkuu
wa Mkoa wa Dar res Salaam, Paul Makonda amefanya ziara kuangalia
utendaji kazi wa magari ya mwendo kasi ambayo yalianza kasi jana Jumanne
na kuelezea maoni yake kwa siku moja ambayo magari hayo yameanza
kufanya kazi.
Makonda
amesema ameshangaa kuona baadhi ya wananchi ambao wanapanda magari hayo
wanagoma kushuka pindi wanapofika kituo cha mwisho.

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Bi. Sophia Mjema wakati alipotembelea kituo cha mabasi yaendayo
haraka kilichopo Kariakoo.
“Wapo
watu wanapanda gari na hawataki kushuka anapanda asubuhi Kimara yeye
anazunguka tu na mimi nimeshangaa kwa mara ya kwanza watu hawa hawapati
hata njaa wala maji yeye anazunguka tu … ukishapanda mara moja shuka
wengine wapande wajifunze,” alisema Makonda.
Aidha
Makonda amewataka wananchi ambao bado wanatumia barabara za mabasi hayo
waache mara moja na tayari kuna askari ambao watakuwa wanasimamia
barabara hizo ili kuhakikisha mbasi hayo pekee ndiyo yanatumia barabara
hiyo.
“Pikipiki,
bajaji, hakuna basi wala gari la mtu binafsi naomba wananchi waelewe
tutakuwa na askari zaidi ya 43 kulinda hizo barabara,” aliongeza
Makonda.
Zaidi unaweza kumsikiliza hapa chini.

Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa DART, Injinia Ronald Lwakatare akizungumza jambo na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati alipokuwa ndani ya
basi liendalo haraka ili kuona jinsi linavyofanya kazi.



No comments:
Post a Comment