Mwimbaji wa nyimbo za injili Ambwene Mwasongwe akiimba katika moja ya kazi zake za kumtumikia Bwana Yesu Kristo.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Waimbaji wa Nyimbo za Injili
nchini wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa kujitolea ikiwa kama sehemu ya
ibada ya kumtumikia Mungu kwa kulitangaza neno lake na si kugeuza kazi
hiyo kuwa mtaji wa biashara.
Hayo yamesemwa na Mwalimu wa
kwaya ya Wateule Elikana Simatiya kutoka kanisa la Anglikani, St. James
lililoko Tabata Segera jiijini Dar es Salaam, maarufu kama kunyata
nyata jina lililotokana na nyimbo ya kunyata nyata aliyoifundisha akiwa
kwaya ya Mennonite.
“Waimbaji wengi wa nyimbo za
injili wameacha kutumikia Mungu na badala yake wamekuwa wakiuunda
vikundi binafsi vya uimbaji ambavyo hutumika kama vyanzo vya fedha na
hualikwa kwenye mikutano ya injili na sherehe mbalimbali kwa malipo
maalum,” alisema Simatiya.
Aidha ameeleza kuwa, uimbaji wa
nyimbo za injili ni wito kama ulivyo wito wa uchungaji lakini hivi sasa
muimbaji wa injili akialikwa katika mikutano ya injili au sherehe huomba
malipo hadi ya shilingi milioni moja.
Simatiya aliongeza kuwa, ziko
gharama ambazo muimbaji anaweza kuomba kupewa kama usafiri kwa ajili ya
kumfikisha eneo husika au malazi na chakula ikiwa atahitajika kulala nje
ya makazi yake, lakini waimbaji wa leo wamebadilisha wito wa kutangaza
injili kwa njia ya uimbaji kuwa biashara.
Hivyo mwalimu huyo amewataka
waimbaji kubadilika kwa kuacha kuharibu kazi ya Mungu na kufanya kazi
hiyo kwa kujitolea kwani wapo wanaopokea uponyaji na wanaotiwa moyo
kupitia nyimbo za injili.
Kwaya ya Wateule inatarajia
kuzindua albamu mpya ijulikanayo kama Wateule tutakwenda siku ya
Jumapili Mei 29, 2016 Tabata Segerea katika kanisa la St. James, ambapo
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul
Makonda,huku wakisindikizwa na waimbaji wa injili ambao ni Ambwene
Mwasongwe, Christina Shusho, Edson Mwasabwite pamoja na kwaya za
Anglikan kutoka Vingunguti na Ukonga.
|
May 25, 2016
WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TUTANGAZE INJILI TUACHE KUIMBA KWA BIASHARA TU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment