![]() |
| Shirikisho la Soka Afrika (CAF),
limewateua waamuzi wanne kuchezesha mchezo Na. 27 kati ya Ethiopia dhidi
ya Ghana kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
vijana 2017 utakaofanyika Uwanja wa Addis Ababa (Gazon Nature), jijini
Addis Ababa huko Ethiopia.
Mchezo huo utaochezwa Mei 22,
2016 majira ya saa 10.00 jioni kwa saa za Ethiopia, utaamualiwa na
Mfaume Ali Nassoro ayesimama katikati wakati walioteuliwa kuwa waamuzi
wa pembeni ni Josephat Deu Bulali (line 1) na Alli Kinduli na mezani
atakuwa Martin Eliphas Sanya. Kamishina wa mchezo huo kwa mujibu wa CAF
ni Julius Elly Mukolwe kutoka Kenya.
|
May 12, 2016
WATANZANIA KUZIAMUA ETHIOPIA, GHANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment