Wafanyakazi
wa kiwanda cha kuchapisha vitabu cha ABANA Printers ltd,kilichopo kata
ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wakiandamana kudai mishahara
na mafao yao wanayodai kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ambayo
yamefikia mil 400 .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
———————————————————–
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAFANYAKAZI
wa kiwanda cha uchapishaji vitabu(ABANA Printers Ltd) kilichopo kata ya
Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ,wanadai fedha za mishahara na
mafao yao kiasi cha sh.mil.400 tangu mwaka 2014 bila mafanikio.
Aidha
wafanyakazi hao waiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati tatizo
hilo kwani wameshapigania haki zao kupitia mahakamani ,wizara,idara na
vyama vinavyojishughulisha kutetea haki za wafanyakazi lakini hakuna
msaada walioupata.
Wameeleza
kuwa hadi sasa wanaishi katika maisha magumu huku wengine wakiwa
wamefukuzwa kwenye nyumba walizopanga na wenzao watatu wamefariki
kutokana na ugonjwa wa moyo.
Hayo
yamejiri jana baada ya wafanyakazi hao kuchukua hatua ya kufanya
maandamano nje ya kiwanda hicho na kisha kumfikishia kilio chao
mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi (CCM)Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif ili
aweze kuwasaidia kulipwa haki zao.
Mwenyekiti
wa tawi la chama cha wafanyakazi tawi la ABANA printers Wilbard Ikigo
,alidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo anajigamba kwa kusema serikali ipo
mkononi mwake hivyo hawezi kuchukuliwa hatua yoyote.
Alisema
ni miaka miwili na nusu sasa tangu watelekezwe na mwajiri wao hali
iliyosababisha kuingia katika mgogoro na mmiliki huyo.
Hata
hivyo Ikigo alisema wameshachukua hatua mbalimbali ikiwemo kufikisha
kero yao CMA ambapo walishinda kesi na kuamuriwa walipwe haki zao .
‘Lakini
mwajiri huyu bado aligomea amri anazopewa tuliamua kwenda kufungua kesi
mahakama kuu ambako tulishinda na iliamuriwa mitambo iliyopo kiwandani
ipigwe mnada ili tuweze kulipwa haki zetu lakini alikiuka tena amri za
mahakama”
“Siku mbili kabla ya mnada
,madalali walijitoa na kushindikana kufanyika mnada huo huku mwajiri
huyo akiendelea kujinadi kuwa serikali iko mkononi mwake na twende
kokote hakuna atakachofanywa”alisema Ikigo.
Alielezea
kuwa hawajui wamiliki wa kiwanda hicho wana nguvu gani hadi
idara,wizara na mahakama zikakiukwa kwa hatua zinazochukuliwa na
kushindwa kuchukuliwa hatua zinazostaki .
Nae
fundi mitambo kiwandani hapo Ally Abdallah alisema walishaandika barua
ya kukutana na waajiri wao ambapo walipokutana nao walikana kuwa
hawawatambui na hawadaiwi na mfanyakazi yoyote.
“Baada
ya hapo tukaenda kwa Paul Makonda wakati alipokuwa mkuu wa wilaya ya
Kindondoni ambako ofisi kuu ya kampuni hii ipo Kinondoni ambapo
alimwandikia barua ya kumpa agizo hadi ikifikia mwezi wa 30,desemba 2015
awe ameshalipa lakini hakulipa.”alisema Abdallah.
Abdallah
alisema hatua nyingine waliyochukua ni kwenda kwa kamishna wa kazi
ambapo aliitwa na kuahidi mwenyewe kuwa atalipa lakini hajalipa hadi
sasa hivyo kamishna huyo aliamua kumshtaki katika mahakama ya kiraia.
Steven Bituro alimuomba Rais
Magufuli kuingilia kati kwa kuwaagiza watendaji wake kuchukua hatua
zinazostahili ili wapate haki zao.
Alisema
kiwanda hicho kwasasa kimefungwa ,badala ya kuendelea kufanya kazi kwa
maslahi ya mtu binafsi na kudidimiza utekelezaji wa kukuza sekta ya
viwanda nchini.
Bituro
alieleza kuwa kiwanda hicho ni muhimu nchini kutokana na kuchapisha
vitabu mbalimbali na ni kiwanda kinachotegemewa kuchapisha vitabu
mashuleni na mitambo yake ni mikubwa lakini kimefungwa kwa maslahi ya
mtu mmoja.
Kwa upande wake msimamizi wa uzalishaji kiwandani humo, Venance Mbamba alikiri ni kweli hawajalipwa madai yao kwa muda mrefu .
Mbamba
alisema ni hatua mbalimbali zimechukuliwa za kisheria pasipo ufumbuzi
na mwajiri ameamua kufunga makufuli kwenye kiwanda hivyo uzalishaji
umesimama kwa mwezi mmoja sasa.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi wilayani Bagamoyo ,alhaj Abdul Sharifu alifika
kiwandani hapo na ameahidi kushirikiana nao bega kwa bega kutatua kero
hiyo.
Alieleza
kuwa kilio hicho kimemgusa kwani dhamira kuu ya rais Magufuli ni kuinua
ajira kwa jamii lakini inashangaza kuona baadhi ya waajiri wanakuwa
wakandamizaji na hawathamini wafanyakazi wao.
Alhaj Sharif aliziomba taasisi za haki za binadamu na serikali kusimamia suala hilo ambalo linawaumiza waajiri na familia zao.
Alisema
ifikie hatua sasa ya kuwachukulia hatua wawekezaji na waajiri
wababaishaji ambao wamekuwa wakijali matumbo yao na kuwatumia watumishi
wao pasipo kuwatahamini.
Juhudi
za kuwatafuta wamiliki wa kampuni hiyo ili waweze kujibu malalamiko
hayo hazikuzaa matunda licha ya kupiga simu zao mara kadhaa.
Kampuni hiyo ya ABANA printers
ltd,ilianza mwaka 2010,ina jumla ya wafanyakazi 45 na inamilikiwa na
wamiliki akiwemo Micael Edler na mkewe Cristina Edler kutoka nchini
Sweden pamoja na mmiliki mzawa Richard Kimwaga Stika .
|
June 30, 2016
WAFANYAKAZI WA ABANA WAANDAMANA KUDAI MIL 400 WANAZODAI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment