KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 24, 2016

WATANZANIA WAASWA KUZINGATIA UMRI KATIKA KUANGALIA FILAMU NA MAIGIZO

index2
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisso akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo tasnia ya filamu nchini katika kuazimisha wiki ya Utumishi wa Umma.
————————————————————
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Watanzania wameaswa kuzingatia umri katika kungalia filamu katika majumba ya sinema na sehemu mbalimbali.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisso wakati akifafanua masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya filamu nchini  kwa  waandishi wa habari.
Bibi Joyce Fisso amesema kuwa Bodi yake inafanya kazi ya kuzipa kiwango kazi za filamu na maigizo ikiwemo umri sahihi wa kuangalia filamu  na hili linapaswa kuzingatiwa na waoneshaji na waangaliaji wa Filamu.
“ Natoa wito kwa watanzania hasa wazazi kuzingatia umri katika kuangalia filamu, ukiona imeandikwa umri wa miaka 18 ujue ni maalum kwa ajili ya umri huo na mtoto chini ya hapo hatakiwa kuangalia kwasababu maudhui ya filamu au maigizo hayo hayamuhusu alisisitiza Bibi. Joyce.
Bibi Joyce Fisso ameongeza kuwa jukumu la kujenga maadili kwa watanzania hasa watoto lipo mikononi mwa wazazi wao na kuwaasa wazazi kuzingatia umri katika kuangali filamu na maigizo mbalimbali ili kupunguza wimbi la mmomonyoko wa maadili nchini.
Aidha Bibi Joyce Fisso ameshauri waandaaji wa filamu na maigizo nchini kuandaa filamu na maagizo yenye maudhui ya watoto  ya kuwajenga katika Mila, Desturi na Tamaduni za kitanzania kwa kuwa ndio kizazi cha baadae na kinatakiwa kulelewa katika maadili mema.
Bodi ya Filamu inapokea filamu na maigizo mbalimbali kwa ajili ya kupata kibali cha kusambazwa na zaidi ya asilimia 70 ya filamu hizo maudhui yake ni mapenzi  hivyo basi jamii inatahadharishwa kuzingatia umri uliowekwa katika filamu na maigizo hayo ili kuepukana na mmomonyoko wa maadili kwa watoto uanaozidi kuongezeka siku hadi siku kwa kuangalia filamu na maigizo yenye maudhui yasiyowahusu.

No comments:

Post a Comment