![]() |
| Micah Johnson |
Mwanamume aliyewafyatulia risasi polisi 12 na kuwaua watano Mjini Dallas nchini Mrekani wakati wa maandamano ya watu weusi dhidi ya polisi wa kizungu amejulikana kwa jina la Micah Xavier Johnson ( 25) ni askari wa akiba na hakuwa na historia ya uhalifu.
Johnson,
anayetokea Mesquite, Texas, mwendo wa dakika 20 hadi Dallas aliwaambia polisi wakati akitekeleza mauaji hayo kuwa yeye ni mzoefu na kwamba alikuwa mwenyewe katika mpango huo uliosababisha mauaji ya polisi.
Alisema amechoshwa na masuala ya Marekani weusi, amechoshwa na maswala ya mauaji ya wamarekani weusi na kwamba alihitaji kuwaua wazungu hasa polisi weupe, alisema mkuu wa Polisi wa Dallas David Brown
![]() |
| Micah Johnson (kulia ) akiwa na kaka yake Tevin (kushoto) na dada yake Nicole (katikati) |




No comments:
Post a Comment