![]() |
TANZIA:
Mwandishi Mwandamizi wa Habari za michezo na burudani wa gazeti la
Majira, Elizabeth Mayemba amefariki dunia usiku wa leo baada ya kuanguka
ghafla nyumbani kwake eneo la Tabata kwa Swai jijini Dar es Salaam.
Taaifa
za awali zinaeleza kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku
huu wa Julai 9.2016,ambapo inaelezwa alikuwa akijisikia kizunguzungu na
ndipo alipopatwa na umauti huo licha ya kukimbizwa Hospitali.
Aidha,
Taarifa kutoka kwa mume wa marehemu, Eliza, Bwana Rogers amebainisha
kuwa…, alipigiwa simu saa mbili usiku na kuambiwa Eliza alisikia
kizunguzungu ghafla na kuanguka chini, alichukuliwa na kupelekwa
hospital baada muda mtu aliyempeleka Eliza hospital alimpigia tena na
kumpa taarifa za Eliza kufariki.
Taarifa nyingine zitatolewa baada ya ndugu wa marehemu kukutaana. RIP Elizabeth Mayemba.
|
July 10, 2016
MWANDISHI WA MAJIRA ELIZABETH MAYEMBA AFARIKI DUNIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nakukumbuka sana mama yangu kipenzi,Mungu akulaze mahali pema peponi
ReplyDelete