KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 1, 2016

TATO YAIOMBA SERIKALI KUANGALIA UPYA KODI ONGEZEKO LA THAMANI

index
Mhmoud Ahmad Arusha
WADAU wa Utalii nchini wameiomba serikali kusitisha utozwaji wa kodi mpya ya thamani ya ongezeko ,VAT , ambayo ni asilimia 25%  kwa kuwa itaua sekta ya utalii nchini.
Hayo yameelezwa leo na wadau wa Utalii kwenye kikao kilichoitishwa na Chama cha waongoza utalii nchini TATO, kujadili hatua ya serikali kuwataka kulipa VAT, asilimia 25% kuanzia Julai mosi mwaka huu.
Wamesema kuwa tayari wageni ambao walitarajiwa kuja nchini kuanzia Augosti mwaka huu na mwakani wamefuta safari zao kutokana na kodi hiyo ya VAT asilimia 25% na sasa wanaenda nchi jirani ya Kenya na hivyo utalii hapa nchini unakufa.
Wamesema wao hawapingi kulipa kodi ila ongezeko hilo ni kubwa hivyo wanamuomba waziri mwenye dhamana ,Profesa Jmanne Maghembe, wakaa meza moja  kujadili mstakabali huo wa ongezeko la kodi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa TATO., Henry Kimambo, akizungumza kwenye kikao hicho amesema tayari wameshawasiliana na kamati ya bunge la jamhuri ya muungano linaloendelea Dodoma, wamekutana na mkuu wa mkoa wa Arusha Felix Ntibenda, ambako amewaahidi kulishughulikia jambo hilo kwa kuwasiliana na mawaziri husika.
Amesema wanashangaa kuona serikali ikiongeza VAT na kuua utalii nchini,  wakati Kenya wameondoa kodi hiyo na huu ni wakati wa ushindani hivyo watalii watakimbilia Kenya .Amesema sekta ya utalii nchini inachangia  pato la taifa kwa asilimia 17% na pia inachangia fedha za kigeni asilimia 33% .
.Ameongeza kuwa wadau wa utalii hawakatai kulipa kodi bali ongezeko hilo ni kubwa kiasi kwamba liaathiri sekta nzima ya utalii na kusababisha makampuni kufunga shughuli hizo.

No comments:

Post a Comment