Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetoa onyo pamoja na kuutaka
uongozi wa Clouds TV kuomba radhi Watanzania kupitia taarifa zake za
habari ndani ya siku tano mfululizo kuanzia leo.
Adhabu hiyo imetolewa leo na kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), baada ya baadhi ya wananchi hususani
watazamaji wa kipindi cha ‘Take One’ kilichorushwa 28 Juni mwaka huu
ambacho kilidaiwa kurusha hewani kipindi hicho kilichozungumzia masuala
ya mapenzi ya jinsia moja (Ushoga) na hivyo kulalamikiwa na wananchi
kwamba kwamba kilikiuka maadili ya taifa kwani kipindi hicho kiliwakwaza
pamoja na kuwasababishia usumbufu wananchi hususani watazamaji kwa
kuwasilisha mada inayozungumzia masuala ya mapenzi ya jinsia moja
(ushoga),
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Joseph Mapunda amesema kuwa
maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wajumbe wa kamati kutafakari maelezo ya
utetezi yaliyotolewa na uongozi wa Clouds TV.


No comments:
Post a Comment