Hafla
ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.

Kamati
hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi
(administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam
Tv).
Tuzo
hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu
yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha
bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la
msimu na mwamuzi bora.
Waliopendekezwa
(nominees) kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya
(Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba) wakati kwa
upande wa kipa bora ni Aishi Manula (Azam), Beno Kakolanya (Tanzania
Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).
Kocha
bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum
Mayanga (Tanzania Prisons). Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji
bora chipukizi ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru
Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
Waliongia
kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma
(Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba). Waamuzi bora
katika kinyang’anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab
Mrope.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewapongeza wateule wote
waliopendekezwa kuwania tuzo hizo. “Kama wadhamini tuna matumaini
makubwa kuwa msisimko wa ligi hii utazidi kuongezeka katika msimu ujao
na kuzidi kuwapatia mashabiki wa soka wanaoifuatilia hapa nchini na nje
ya nchi.”
Alisema
Vodacom itaendelea kudhamini ligi hiyo kubwa ya soka nchini ili
kutekeleza moja ya malengo yao ya kuibua na kuendeleza vipaji vya
wachezaji nchini. Pia kuwawezesha wachezaji kujipatia ajira na kuboresha
maisha yao kupitia sekta ya michezo bila kusahau kuwapatia burudani
wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment