Kiongozi Mkuu wa ACT, Zitto Kabwe tayari ameondoka nchini kuelekea nchini Marekani ambao alialikwa na mgombea urais wa nchi hiyo, Hillary Clinton kuhudhuria mkutano mkuu wa chama cha Democratic.
Akiwa katika mkutano huo, Zitto anataraji kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka mataifa mbalimbali duniani kuhusu hali za kiasi katika mataifa yao.
Pia akiwa nchini Marekani anataraji kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla lakini pia kuanza kufanya maandalizi ya ufunguzi wa tawi la wanachama wa ACT Diaspora.
Nafasi abayo ameipata Zitto inaonekana kuwa fursa ya kipekee katika maisha yake ya kisiasa kwani mkutano atakaohudhuria ndiyo utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombe urais kupitia chama cha Democratic.