Kanisa
la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, chini ya
Mchungaji kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola, linapenda kuwakaribisha
watu wote kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya na la kisasa
linalotarajiwa kujengwa katika viwanja vya kanisa hilo.
Harambee
hiyo inatarajiwa kufanyika kesho jumapili Agosti 28,2016 kanisani hapo
ambapo watu wote wakiwemo waumini na viongozi wa Madhehebu mbalimbali,
Viongozi wa Serikali na Taasisi binafsi, wanakaribishwa ili kuungana na
viongozi na waumini wa Kanisa hilo katika kushiriki kwenye harambee
hiyo.
Kumbuka
“Bwana Hufurahi Anapojengewa Hekalu Lenye Kufana” hivyo utabarikiwa
ikiwa utashiriki katika harambee hiyo. Kwa mawasiliano zaidi, tumia
nambari za simu; 076774 90 40 AU 0787 74 90 40.
No comments:
Post a Comment