WAKUU
wa wilaya wastaafu, walioteuliwa wakati wa Serikali ya awamu ya nne, wameunda Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS), ikiwa ni
moja ya maazimio waliyotoka yao baada ya semina ya
mafunzo ya siku mbili, iliyolenga kuwaelimisha namna bora ya kuwa
wajasiriamali.
Akitangaza
azimio hilo, mwishoni mwa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa
Sekretariati ya wakuu hao wastaafu, Crispin Meela, alisema, wajumbe 10
wamechaguliwa na wana semina hao ili kushughulikia utaratibu mzima wa
kuanzishwa kwa SACCOS hiyo haraka iwezekanavyo.
Wajumbe
wa Kamati ya muda ya kusimamia mambo hayo ni pamoja na Ramadhan Maneno
(Mwenyekiti), Betty Mkwasa (Katibu), Crispin Meela, Erasto Sima, Geogina
Bundala, Farida Mgomi, Said Amanzi, Fatma Ally, Muhingo Rweyemamu na Manzie
Mangochie.
Kwenye
mafunzo hayo Wakuu hao wa wilaya wastaafu, waliweza kupata elimu kutoka kwa
wataalamu mbalimbali wakiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, Beng’ Issa, na wataalamu wa Saikolojia, na Wajasiriamali
wenyewe kama vile Eric Shigongo.
Akifunga
mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, ametoa changamoto kwa wakuu
hao wanaokadiriwa kufikia 100 na ambao wamejiunga uanachama wa Mfuko huo kupitia
mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kuwa uamuzi wao utawakwamua kiuchumi na
wanachotakiwa ni kuwa na mpango kamambe utakaoweza kutekelezeka kwa ufanisi
mkubwa.
“PSPF
kama shirika lingine lolote lile la kutoa huduma za Pensehni na za kifedha,
umoja huo ni fursa kubwa kwa Mfuko na ndio maana umeamua kuwaunga mkono ili mmfikie azma yenu ya kuanzisha SACCOS hiyo”.
Alisema.
HABARI KATIKA PICHA
HABARI KATIKA PICHA
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akitoa mada juu ya
ujasiriamali kwa Wakuu wa Wilaya wastaafu, wakati wa semina ya mafunzo ya
ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao
makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 16, 2016.
Mwenyekiti wa Wakuu wa wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (watatu
waliokaa), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji,
(wapili waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, George
Yambesi, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu,
(wakwanza kushoto waliokaa) na Mwenyekiti wa Wakuu hao wa Wilaya
wastaafu, Ramadhan Maneno, (wakwanza kulia waliokaa) wakiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya wastaafu hao






No comments:
Post a Comment