KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 19, 2016

WAZIRI MKUU:UKAGUZI WA WANAFUNZI HEWA UFANYIKE NCHI NZIMA



WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (pichani) amewaagiza wakuu wa wilaya na maofisa elimu nchini, wafanye ukaguzi katika shule ili kubaini wanafunzi hewa kwenye mpango wa elimu bure.
Katika hatua nyingine, serikali imesema itawavua madaraka wakuu wa shule ambao hawataki kubadilika na kuwatimua walimu wote wanaotumia dawa za kulevya ikiwemo bangi, wasio na sifa ya kufundisha na wenye vyeti bandia kwani wamekuwa chanzo cha kudorora kwa ufaulu katika shule kongwe nchini.
Aidha, imeanza kutoa Sh bilioni 21 kila mwezi kama ruzuku ya uendeshaji shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka kwa ajili ya wakuu wa shule na walimu wakuu.
Kuhusu kufanyika kwa ukaguzi katika shule ili kubaini wanafunzi hewa kwenye mpango wa Elimu Bure, Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana alipokutana na watumishi na viongozi wa Manispaa ya Ilala katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Kila mwezi serikali inapeleka shule zaidi ya shilingi bilioni 18 kugharimia elimu bure na sasa tumeanza kuona udanganyifu katika sekta ya elimu kwa kuwa na wanafunzi hewa. Wakuu wa Wilaya na Maofisa Elimu nendeni mkafanye ukaguzi ili mpate takwimu sahihi. “Mkiona takwimu ziwachanganya ni lazima mtoke maofisini na kwenda katika shule zilizo kwenye mpango wa elimu bure mkafanye uhakiki wa idadi ya wanafunzi,” alionya

No comments:

Post a Comment