
Shehena ya dawa zilizoagizwa na S
erikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwa zimehifadhiwa kwenye Bohari kuu
Maruhubi kabla ya kusambazwa katika hospitali na vituo vya Afya.

Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa
Zanzibar Zahran Ali Hamad akimkabidhi dawa Daktari msaidizi wa
Hospitali ya Wilaya Makunduchi Asha Salum Hassa (wa pili kulia) kwa
ajili ya Hospitali hiyo.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
…………………………………………………….
Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha kwamba Hospitali na Vituo
vyote vya afya vinapatiwa dawa zote muhimu kwa ajili ya wananchi.
Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa
Zanzibar Zahran Ali Hamada amesema Serikali tayari imeidhinisha
shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kununulia dawa na Wizara imeshatumia
shilingi milioni 600 kununua dawa ambazo zitatosha katika kipindi cha
miezi mitatu ijayo.
Amesema katika mwaka wa fedha
2016/17 Serikali imetenga shilingi bilioni tano kwa ajili ya kununulia
dawa ambazo zinakidhi mahitaji ya wananchi katika kuendeleza azma ya
Serikali ya kutoa huduma za afya kwa wananchi bila malipo.
Akisambaza dawa hizo katika
Hospitali na vituo vya afya, Zahran amewaeeleza wafanyakazi kuwa
Serikali imetumia fedha nyingi kununua dawa hivyo amewataka kuzitunza
na kuwapa wananchi kwa mujibu wa mahitaji yao.
“Hakuna haja ya kuweka akiba dawa
wapeni wananchi, dawa zipo zakutosha na utaratibu wa kuagiza nyengine
umeshaanza, ”alisisitiza Mkurugenzi wa Bohari Kuu.
Alisema Wizara itaandaa utaratibu
wa kufuatilia matumizi ya dawa hizo ili kuhakikisha zinawafikia
wananchi na amewashauri viongozi shehia na wananchi kwa jumla kuwa
walinzi wa dawa hizo.
Daktari Msaidizi wa Hospitali ya
Makunduchi Dkt. Asha Salum Hassan amesema hali ya dawa hivi sasa
inaridhisha na dawa nyingi muhimu zinapatikana isipokuwa dawa za maumivu
na Anti biotic zinatumika kwa wingi hivyo baadhi ya wakati zinakwisha
bila ya kuingizwa nyengine.
Ameahidi kuwa dawa hizo
zitatumika kama zilivyokusudiwa kwa ajili ya wananchi na atahakikisha
kuwa hakutatokea ubadhirifu wowote ulio nje ya utaratibu uliopangwa na
Wizara.


No comments:
Post a Comment