KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 5, 2016

BREAKING NEWS: HATIMAYE WANAOMPIGA PROFESA LIPUMBA NA MSAJILI WATINGA MAHAKAMA KUU KUFUNGUA KESI LEO

 Wakati sakata la nani ni nani ndani ya chama cha CUF Likiendelea kuchukua sura mpya kila kukicha hatimaye leo sakata hilo limetua Mahakama  Kuu ya  Tanzania likiwa na sura ya kupinga kile ambacho kinadaiwa kufanywa naMwenyekiti wa wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba.

Katika Makahakama Kuu Jijini  Dar es salaam mtandao huu umeshuhudia Wakili wa chama hicho Juma Nassor  akiwa  mahakamani hapo kuiwakilisha Bodi ya Wadhamini wa chama hicho ambao ndio wanafungua kesi hiyo, wakitaka Mahakama hiyo kuweka ziuo maalum kwa Msajili wa Vyama Vyavya Siasa kuacha kufanya kazi nje ya mipaka yake ambapo pia wanamlalamikia Msajili kuingilia maswala ya chama hicho kinyume na utaratibu.

Akizungumza na Wanahabari nje ya Mahakama Kuu Juma Nassor amesema kuwa mbali na kuweka zuio kwa Msajili pia kesi hiyo imewalenga waliokuwa wanachama 12 wa CUF wakiongozwa na Profesa Lipumba.

Hadi mtandao huu unaleta taarifa hii taratibu za kufungua keshi hiyo zilikuwa zinaendelea HABARI NA PICHA KWA HISANI YA HABARI 24 BLOG

No comments:

Post a Comment