Mkurugenzi wa TEA Joel Laurent
katikati akiangalia darasa la Tehama Computer ambazo baadhi zilitolewa
kama msaada na TEA kwa shule hiyo.
……………………………………………………..
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa jimbo la Mafinga mjini
Cosato Chumi amewataka wananchi kuendelea kujituma kufanya kazi wakati
akitafuta ufumbumzi wa kero na changamoto mbalimbali za jimbo hilo
jimpya.
Aliyasema hayo alipokutana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bw Joel Laurent katika
Shule ya makalala yenye mahitaji maalumu huku lengo likiwa ni
kumuonyesha mkurugenzi huyo jinsi hali ilivyombaya ya kitaalum na
mazingira yalivyo magumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
“Ninajitahidi kufanya kila
kinachowezekana ili mradi kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la
mafinga na kuleta maendeleo kadili ninavyoweza” alisema chumi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Elim Tanzania Bw Joel Laurent alisema kuwa atatuma timu
yake ya wataalam kwa ajili ya kufanya tathimini ya mahitaji ya
miundombinu katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Makalala iliyopo
Mafinga.
Bw Laurent aliyasema hayo siku Alhamis alipoitembelea Shule hiyo kufuatia ombi la Mbunge wa Mafinga Mjini.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba
TEA pamoja na mambo mengine Ina wajibu wa kusaidia miundombinu na vifaa
saidizi vya kufundishia na kujifunzia na kwamba Mwaka huu wataelekeza
nguvu katika Shule za mahitaji maalum kama Makalala na kwa wanafunzi
wenye mahitaji maalum katika Shule za kawaida.
Shule hiyo yenye uwezo wa
kuhudumia wanafunzi 48 wa bweni wenye ulemavu wa akili, wenye ualbno na
wenye uono hafifu inakaribiwa na uhaba wa Bweni ambapo kwa Sasa
wanafunzi wanalazimika kulala mpaka watoto Sita katika baadhi ya vyumba.
Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema kuwa
anaishukuru TEA kwa kuitikia wito wa kuitembele shule hiyo yenye
mahitaji maalumu na kuomba serikali kuwapa ushirikiano kutatua
changamoto za shule ya makalala sambamba na kuwaomba wada wengine
kuendelea kuisadia shule hiyo.Wiki iliyopita TEA ilitoa msaada wa vifaa visaidizi vya kusomea katika shule ya Ilboru sambamba na kukabidhi fimbo nyeupe mkoani Mbeya.



No comments:
Post a Comment