
Mkuu
wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akishirikiana na
wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Temeke kukata utepe kuashiria uzinduzi
wa Tawi la Temeke jijini Dar es Salaam.
BENKI
ya Exim imefanya maboresho ya huduma zinazotolewa kwa wateja wake wa
maeneo ya Temeke, jijini Dar es Salaam kwa kufungua tawi jipya ambalo
lina maboresho mengi tofauti na jengo ambalo walikuwa wakilitumia awali.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim,
Seleman Mponda amesema kwasasa wamedhamiria kuboresha huduma zao katika
maeneo mbalimbali na kuahidi wateja kuendelea kuwapatia huduma bora.
“Benki
yetu inaendelea kufanya vizuri na tumejipanga kuendelea kuboresha
huduma zetu, mwanzoni tulikuwa sehemu nyingine na wateja wetu walikuwa
wakituuliza lini tutahamia sehemu iliyo na nafasi nzuri ya kutoa huduma
na sasa tumeipata,” alisema Mponda.


No comments:
Post a Comment