![]() |
| Baada
ya kumalizika kwa mchezo wa EPL kati ya Liverpool iliyokuwa mwenyeji wa
Manchester United na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana, kocha wa
Man United, Jose Mourinho amezungumza kuhusu mchezo huo.
Mourinho
amesema Liverpool alicheza vizuri lakini walifanikiwa kuwadhibiti na
kuwafanya kushindwa kupata goli lakini pia wapinzani wao walikuwa na
washambuliaji wa kawaida ambao walishindwa kuwaletea madhara licha ya
kumiliki mpira kwa muda mrefu.
“Liverpool
ni timu nzuri sana, unaweza kusema ni jambo la mwisho la ajabu
wanafanya katika kushambulia, lakini wana timu ambayo inacheza na
kufikiri jinsi ya kuzuia,
“Tuliwazuia
wao kucheza lakini bado walicheza vizuri katika eneo la kuzuia.
Walimchezesha Emre Can na Jordan Henderson kwa sababu maalumu na
walifanya hivyo kwa dakika 90. Walikuwa na wachezaji wa kawaida katika
eneo la kushambulia lakini Can na Henderson walikuwa makini sana katika
eneo lao,” alisema na kuongeza.
“Msimu
uliopita United ilishinda hapa na Liverpool walikuwa na mashuti 14. Leo
mangapi? mawili. Wameongoza takwimu kwa asilimia 65 na mashuti mawili.
Jambo muhimu ni Liverpool sio sehemu yetu, ni matatizo yao, sio kosa
letu”
|
October 18, 2016
MANENO YA MOURINHO BAADA YA SARE NA LIVERPOOL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment