Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji
MBUNGE wa jimbo la
Rufiji, mkoani Pwani, Mohammed Mchengelwa ameahidi kula sahani moja na
baadhi ya viongozi wakiwemo wa vijiji ambao wanadaiwa kushirikiana na
wafugaji kuingiza mifugo kiholela jimboni hapo.

Mbali na hilo amesema amejipanga kuvalia njuga suala la migogoro ya ardhi inayotokana na jamii ya wafugaji na wakulima.
Ameeleza pande hizo
zimekuwa zikisigana mara kwa mara wakigombania maeneo hali
inayosababisha kutokea kwa vurugu ambapo wakati mwingine hupelekea
uvunjifu wa amani.
Aidha Mchengelwa
alisema kuwepo kwa migogoro ya ardhi kwa wakulima na wafugaji katika
halmashauri ya Rufiji kunatokana na baadhi ya wafugaji kuamua kuvunja
sheria na taratibu zilizopo.

No comments:
Post a Comment