Judith Mhina na Lilian Lundo – MAELEZO
Serikali kupitia Mradi wa Mpango
wa Kuboresha Elimu – EQUIP (Education Quality Improvement Programme)
imeendelea kuboresha mfumo wa Elimu hapa nchini katika nyanja ya mitaala
kwa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tatu, uongozi bora katika
shule za msingi pamoja na mifumo ya utoaji taarifa na takwimu sahihi.
Mratibu wa mradi huo hapa nchini
Bw Johan Bentinck, amesema hayo leo jijini, Dar es Salaam alipokuwa
akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo na namna ambavyo umefanikiwa
katika kuboresha Elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa
saba hapa nchini.
Mradi huo umetoa fursa kwa walimu
kupata mafunzo ya namna ya ufundishaji bora utakaomuwezesha mwanafunzi
wa darasa la kwanza hadi la tatu kujua kusoma, kuandika na kuhesabu
ndani ya muda mfupi na kwa ufasaha.
Aidha kupitia mradi huo
ufundishaji darasa la Kwanza mpaka la Nne umeboreshwa ambapo mwanafunzi
anaweza kuunganisha maneno kwa kutumia sauti. Vile vile kumekuwepo na
njia nyingine za kufundisha kupitia nyimbo na michezo mbalimbali kwa
wanafunzi wa madarasa ya awali.
Pia mradi umewezesha kuanzishwa
kwa madarasa ya awali ambayo hayakuwepo katika shule za msingi zilizoko
vijijini. Wanafunzi wa madarasa hayo wamekuwa wakifundishwa na walimu wa
kujitolea kwa muda wa wiki 12 na baada ya hapo hujiunga na darasa la
Kwanza.
Aidha mradi huo umeleta mafanikio
makubwa katika sekta ya Elimu hapa nchini ambapo kasi ya ya kutamka
maandiko kwa mwanafunzi wa darasa la Kwanza mpaka la Tatu ilikuwa 21.3
mwaka 2014 na sasa ni 30.0
“Mradi huo kwa sasa unahusisha
mikoa ya Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara na Lindi huku
mikoa mingine miwili ya Katavi na Singida inategemea kuongezwa mwaka
2017,” alifafanua Bentinck



No comments:
Post a Comment