KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 3, 2016

MKURUGENZI ARUSHA AFAFANUA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA JENGO LA UTAWALA KALIUA

Na Woinde Shizza,Arusha

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Athumani Kahamia ametoa
ufafanuzi kuhusu tuhuma ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha sh, 500 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua na kusema kwamba fedha hadi anahamishwa fedha hizo hazikuwahi kuletwa katika halmashauri hiyo kutoka serikali kuu.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma mbalimbali zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini ambapo Kahamia anatuhumiwa kutumia kiasi hicho cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Kaliua wakati akiwa mkurugenzi wa Kaliua kabla ya kuhamishiwa jijini Arusha.

Akihojiwa na mwandishi Wa Habari hizi Kahamia alisema kwamba aliripoti mnamo febuari 2015 katika halmashauri hiyo na kukuta ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea ambapo katika bajeti ya halmashauri ya Kaliua mwaka wa fedha 2015/16 waliomba fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo katika awamu ya kwanza lakini serikali haikuleta pesa hizo.

No comments:

Post a Comment