
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni Mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.
………………..
Na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe amefungua mafunzo ya upelelezi kwa askari 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni, mkoa ambao Jeshi la polisi nchini limeuchangua kuwa eneo la mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha usalama wa jamii uliozinduliwa katika viwanja vya Biafra kinondoni jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo ya upelelezi ya miezi miwili yamefunguliwa katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu kilichopo mkoani morogoro yamefadhiliwa na taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Hanns Sidel inayotekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa huo, Dkt Kebwe alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha cha Jeshi la Polisi kuamua kuchangua mkoa wa Morogoro kufanyia mafunzo hayo na pia kumchagua yeye kuwa mgeni rasmi.
Dkt Kabwe alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi ngumu wanayoifanya ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao na aliwataka askari wanaopata mafunzo hayo katika chuo cha maafisa wa polisi kidatu kutumia weledi na taaluma hiyo watakayoipta kutatua kero za wananchi zinazotokana na ucheleweshaji wa upelelezi .
“ Nimefurahi sana kusikia kuwa mafunzo haya yanalenga kuharakisha upelelezi na kesi yoyote itakuwa inapelelezwa itakuwa imekamilika ndani ya siku sitini” alisema Dkt Kebwe.
Mapema akitoa utangulizi wa mafunzo hayo, mkuu wa kitengo cha kinachoratibu utekelezwaji wa mpango wa Jeshi la Polisi wa kuboresha usalama wa jamii, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Godluck Mongi alisema kuwa mafunzo hayo ya upelelezi yataleta mafanikio makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha upelelezi wa kesi .
Aliongeza kuwa lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 askari wote upelelezi wawe wamepata mafunzo hayo na hatimaye kupuza kero ya uhalifu katika mkoa wa kinondoni kwa asilimia 10%


No comments:
Post a Comment