KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 4, 2016

MOISE KATUMBI ASEMA ATAREJEA DRC HIVI KARIBUNI

Image result for moise katumbiUchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utacheleweshwa hadi mwaka 2018 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.
Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani kwa miaka 15 lakini katiba haimruhusu kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Vyama vya upinzani vimekuwa vikimlaumu Rais Kabila, kwa makusudi kuchelewesha uchaguzi, ili aendelee kuwa madarakani hata wakati muhula wake utakapomalizika, mwezi Desemba.
Salim Kikeke alizungumza na kiongozi wa chama kimoja cha Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi na kumuuliza kama atarudi nyumbani Congo.Moise kwa upande wake anasema atarudi na kushiriki shughuli mbalimbali za kisiasa kama raia wa Congo, kwa sasa yuko Afrika Kusini alikokwenda kutibiwa huku Mahakama moja nchini humo iliwa imemuhukumu miaja mitatu jela kwa kosa la kununua nyumba kinyume cha sheria-BBC

No comments:

Post a Comment