Na Mahmoud Ahmad Longido
Mkurugenzi halmashauri ya Longido
bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi
wa polisi mtendaji wa kata ya Egirai Lumbwa Wilayani Londigo bwana
Paulo Luka kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa madarasa ya
shule ya sekondari Natroni Flamingo.
Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya
wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai Lumbwa kuikata taarifa
iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha ujenzi mpaka kukamilika
utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango ya awali ilikuwa
milioni 12 na kati ya hiyo milioni 4 tu ndio ilikuwa michango ya
wananchi.
Wananchi hao walimweleza Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali
walizonazo baada yakufanya ziara katika kijiji hicho , walisema kuwa
wao wanavyojua wamechanga zaidi ya fedha zilizotajwa kwenye taarifa
hiyo.
Hivyo Gambo alimtaka Mkaguzi wa
ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi ya fedha hizo, akifafanua
Bi. Mwajuma mdaira alisema alifanya ukaguzi na kugundua kuwa fedha
zilizokusanywa kwa njia ya michango ilikuwa milioni 95 na milioni 50
kati ya hizo zilitumika kwenye marekebisho ya majengo ya shule japo
hakukuwa na mikata yoyote iliyoingiwa kati ya shule na mkandarasi.
Pia fedha hizo zilitumika bila
kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri, na kuna wawekezaji 2 ambao
ni Winget Windros Safari walichangia mifuko 200 ya simenti na mingine
200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia ujenzi lakini mifuko 144
kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika matumizi yake lakini
bado anaendelea na ukaguzi zaidi.
Hivyo kumpelekea Mkuu wa Mkoa
Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji huyo kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana yake tu na hapo hapo
akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata mtendaji huyo nakumpeleka
kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya ubadhilifu huo.
Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo yupo
katika ziara ya kikazi Wilayani Longido kwa mda wa siku 5 ilikujionea
maendeleo na pia kusiliza Changamoto mbalimbali za wananchi wa Wilaya
hiyo.


No comments:
Post a Comment