
Katibu wa Kamati ya Muafaka ya
Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akizungumza na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa kamati
hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga kuhusu ukodishwaji wa Nembo ya
timu hiyo.

Katibu wa Kamati ya Muafaka ya
Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akionyesha baadhi ya vipengele
vilivyokosewa katika kukodisha timu ya Yanga kwa na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa
kamati hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga kuhusu ukodishwaji wa
Nembo ya timu hiyo.
…………………………………………………………….
Kabla ya kufanyika mkutano Mkuu
wa dharura wa klabu ya Yanga,siku ya Leo kamati ya Mwafaka wa wazee wa
timu hiyo imezungumza na waandishi wa habari kuhusu maamuzi ya
mwenyekiti Yusuf Manji kutaka kuitumia nembo ya Yanga kwa miaka 10 ili
awe mmiliki halali.
Akizungumza
katibu wa kamati hiyo Ibrahim Akilimali ,amesema kuwa kitu ambacho
anataka kukifanya Manji kinapelekea kwenye vurugu kubwa kuzidi hata ile
ambayo ilishawahi kutokea kipindi cha nyuma kwani atawagawa wanachama
pamoja na mashabiki wanaotaka mfumo huo na wale wanaokataa mfumo huo
pia.
“Sisi
hatutaki kabisa kurudi kule ambapo tulipokuwepo katika migogoro ya
miaka nane na mwaka 2002 ndipo tulipata mwafaka wa suluhisho na
kukubaliana kuwa tutumie jina ambalo lilidhiwa na waasisi wetu na kuwa
na Yanga sport club na Yanga Cooperation”alisema Akilimali
Aidha
amesema kuwa Yanga kampuni ilikufa na tukaweka utaratibu wa kuwa na
hisa ambazo ni 51 asilimia ni ya Yanga pamoja na asilimia 49 ni ya
wanachama na tulizunguka mikoa mingi mno kwa ajili ya kuondoa
migogoro,kesi na kuomba radhi wanachama wa klabu hiyo.
Hata
hivyo amesema kuwa tulukuwa na mwanasheria ambaye alikuwa mwenyekiti
mpaka anamaliza muda wake aliiachia Yanga Mil 200 na hapo hapo tukampata
tena mwanasheria mzuri bahati mbaya Nchunga alijiuzulu baada ya kukaa
miaka miwili na hatimaye tukampta bwana Manji naye akaongoza miaka
miwili kwa sababu ya mahaba yetu ikabidi tuikanyange katiba kwa
kumuongezea muda tena na tulimchagua tena.
“Sasa
tunashangaa haijapita hata miezi nane linakuja deni la billioni 11 na
laki 6 kitu ambacho kimetushutusha mno wanayanga na pia limekuja swala
la kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na nembo ya klabu kwa muda wa mika
10 ila sisi tunasema kuwa Yanga ni kubwa sana na haiwezi kukodishwa kama
masufuri ya kwenda msibani na mimi na wazee wa kamati kwa pamoja
tunasema hatukubaliani na jambo hilo kwa asilimia mia”alisema Akilimali
Kwa
upande wa aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya jiji la Dar es salaam ya
Yanga,Mohammed Msumi amesema kuwa kutokana na Manji kuwa na mahitaji
makubwa na timu hiyo ni vyema akakaa pembeni au kuanzisha timu yake
mwenyewe na kuiacha Yanga ili iweze kujiendesha kwa mfumo wa kisasa.
“Tujiulize
maswali ivi ni kwanini anataka mchakato huu ufanyike haraka huku
alishawahi kusema kuwa Yanga inajiendesha kwa hasara ni mtu gani huyu
anakaa sehemu ya aina hiyo na kama hawezi kufuata utaratibu wa klabu na
kushindwa kufuata katiba kama anauwezo aanzishe timu yake na kuacha
kutumia pesa zake kwa mabavu iili aichukue Yanga”alisema Msumari


No comments:
Post a Comment