Baada
ya mashabiki wa Simba kuvunja viti vya uwanja wa taifa katika mchezo wa
Simba na Yanga uliopigwa jana Jumamosi na kumalizika kwa sare ya goli
ya moja kwa moja, serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo, Nape Nnauye
amepiga marufuku uwanja wa taifa kutumika na timu za Yanga na Simba.
Waziri
Nape amefanya maamuzi hayo baada ya leo Jumapili kufanya ziara katika
uwanja wa taifa kushuhudia uharibifu wa viti uliotokea jana, amesema
kutokana na tukio ambalo limejitokeza, kuanzia sasa michezo ya timu hizo
haitaruhusiwa kufanyika katika uwanja huo hadi pale ambapo serikali
itawaruhusu.
![]() |
| Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini iliyofanyika mara baada ya mechi wa jana kati ya Simba na Yanga na jumla ya mageti manne yamevunjwa na viti1781 vimeong’olewa katika Uwanja wa Taifa. |
![]() |
| Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016. |
“Uwanja
huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka pale tutakapoamua vinginevyo
hapo baadae hawatatumia uwanja huu watafute viwanja vingine, sababu hapa
kuna pesa za walipa kodi, kuna pesa za watanzania,
![]() |
| Eneo liliong’olewa viti katika Uwanja wa Taifa katika mechi ya Simba na Yanga iliyofanyika Oktoba Mosi. Habari na Picha na Raymond Mushumbusi - MAELEZO |
“Wanaotakiwa
kutumia uwanja huu ukiwa mzuri kama ulivyo ni wengi kuliko Yanga na
Simba, wapo wengine ambao ni wastaarabu wanaweza kutumia uwanja huu,”
amesema Waziri Nape.





No comments:
Post a Comment