KAMPUNI
ya simu za mikononi ya Smart,inatarajia kutoa huduma ya bure ya
mtandao wa Wifi katika tamasha la Kandanda Day,litakalofanyika
leo,katika Uwanja wa Jakaya M Kikwete Youth Park,Kidogo Chekundu.
Mratibu
wa tamasha hilo,Fatma Dahir,alisema kwamba maandalizi kuelekea tamasha
hilo yamekamilika na wanaishukuru kampuni ya Smart kwa kuwawekea
wanakandanda huduma ya kuperuzi mtandao wa intaneti bure wakiwa
uwanjani.
“Tunapenda
kuwatangazia wanakandanda wote kuwa maandalizi yamekamilika kila
kitu,halikadhalika tunapenda pia kuishukuru kampuni ya Smart,kwa kuamua
kusherehesha tamasha letu kwa kuwawekea huduma ya ‘free wifi’ kwa
watakaohudhuria,”alisema Fatma na kuongeza:
“Halikadhalika,napenda
pia kusisitiza timu shiriki ambazo ni Akiba Commercial bank,Taswa
Fc,Coca Cola,Smart,Dar City Fc,Team Dizo Moja na Team Ismail,zijitahidi
kuwahi mapema,ili tuweze kufanikisha lengo letu katika muda tuliopanga.”
Tamasha
hilo ambalo lengo lake kuu ni kuchangia madawati kwa shule teule ya
msingi ya Msumi,linapambwa na kampuni ya matairi ya Bin Slum Tyres
Ltd,Smart,Coca Cola,Galacha na kituo cha House of Blue Hope.



No comments:
Post a Comment