
Mkurugenzi wa Global Publishers
Bw.Erick Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya
mchuano mkali nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha
Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es
salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa
mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa
kawaida.

Picha ya pamoja ya Timu
iliyoibuka washindi wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya
Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam
tarehe 14.10.2016. Ushindi ulipatikana kwa mikwaju ya Penati baada ya
kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida.

Baadhi ya viongozi wa Jeshi la
Magereza na wageni mbalimbali wakiwa wameketi meza kuu katika gerezani
Ukonga wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere
Nchini lililofanyika gerezani humo tarehe 14.10.2016

Baadhi ya viongozi wa Jeshi la
Magereza na wageni mbalimbali wakishiriki chakula cha mchana pamoja na
wafungwa (hawapo pichani) gerezani Ukonga wakati wa Tamasha la Michezo
katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani humo
tarehe 14.10.2016

Baadhi ya wachezaji wa timu
iliyoibuka mshindi wakishangilia baada ya kupachika bao la kusawazisha
katika dakika mbili za mwisho na kufanya mchezo kuwa 2-2 na kisha
kuingia katika mikwaju ya penati zilizowa ushindi wachezaji wenye uzi
mwekundu wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere
nchini lililofanyika ndani ya gereza la Ukonga jijini Dar es salaam
tarehe 14.10.2016

Kepteni wa Timu iliyoshinda
Johnson Nguza (Papii Kocha) akibeba kombe kwa niaba ya timu yake baada
ya kulipokea toka kwa Mgeni Rasmi Erick Shigongo wakati wa Tamasha la
Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani
Ukonga jijini Dar es salaam, tarehe 14.10.2016

Johnson Nguza aka Papii Kocha
akitumbuiza kwa pamoja na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa Tamasha
la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika
gerezani Ukonga jijini Dar es salaam, tarehe 14.10.2016

Mkurugenzi wa Global Publshers
akisalimia wafungwa (hawapo pichani) mara alipowasili gerezani Ukonga
katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere.(Nyerere Day) leo tarehe
14, 10, 2016 jijini Dar es salaam.

Baadhi ya Wafungwa walioshiriki
katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Tamasha la Michezo katika
kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini
Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wlio kushoto.

Baadhi ya Wafungwa walioshiriki
katika mchezo wa kushikana mieleka wakati wa Tamasha la Michezo la
kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini
Dare es salaam tarehe 14.10.2016

Mkurugenzi wa Global Publishers
Bw.Erick Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya
mchuano mkali nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha
Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es
salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa
mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa
kawaida.
………………………………………………………
Na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza
Katika kuadhimisha miaka 17 ya
kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere Gereza Kuu Ukonga kwa
kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya Tamasha la
michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.
Akiongea katika Tamasha hilo
Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi Bwana Erick
Shigongo amewaambia wafungwa kuwa dhimra ya ujio wao gereza ni katika
kuonesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao
gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.
Bwana Shigongo aliwatia moyo
wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya
kubadilika na kuwa raia wema. “Kila mwanadamu anaowajibu wa kubadili
maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi
na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka kwanini wewe
ushindwe?”
Aliongeza “ najua wengi wenu mko
hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwakuwa mmehukumiwa, hizini hukumu za
wanadamu, mnaouwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku
mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili
maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu
atakuongoza alisisitiza Shigongo.
Wadau wengine walioungana na
Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za
Binadamu Nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na ndugu
Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza Ukonga) ambao kwa pamoja
walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao ikiwemo vifaa vya,
sabuni,soda kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika
mpira wa miguu.
Katika Tamasha hilo wafungwa
walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika
kijiti, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti,
kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya
uchekeshaji, kuimba kwa mtindo kufokafoka, ngoma za jadi na burudani
kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga pepeta.


No comments:
Post a Comment