![]() |
Kampuni
ya magari ya Toyota Tanzania Limited imezindua jumba la maonyesho la
kisasa kwenye makao makuu yake jijini Dar es salam ikiwa ni jitihada za
kuboresha huduma kwa wateja.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki,
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Bw. Mahmood
Karimjee alisema “Uzinduzi wa jumba hilo la maonyesho unaleta zama mpya
katika safari ya Toyota Tanzania, inadhiirisha azma ya Karimjee Group
katika kutoa huduma bora kwa wateja. Wateja sasa watafaidika na huduma
zilizoboreshwa na bora zaidi kimataifa na tunatarajia watafurahia huduma
hii kwa miaka mingi ijayo”.
Jumba
hilo kubwa la magari ya Toyota yanayotumika zaidi hapa nchini
limeboreshwa kwa kuwekewa huduma nyingi za kisasa kama kumbi za mikutano
zenye vifaa vya kisasa ili kuendana na viwango vya kimataifa na
litatumika kama maonyesho ya magari ya Toyota hususani aina mpya za
magari hayo yakiwemo yale yaliyozinduliwa hivi karibuni kama Hilux pick
mpya, Fortuner SUV na Landcruiser VXR.
|
October 24, 2016
TOYOTA TANZANIA YAZINDUA JUMBA LA MAONYESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment