Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
ASKARI
polisi katika kituo cha polisi Mlandizi,Kibaha Vijijini mkoani
Pwani,wanakabiliwa na changamoto ya kuishi uraiani kwenye nyumba za
kupanga kutokana na ukosefu wa makazi kwa ajili yao.
Ukosefu
wa nyumba za polisi hao husababisha kuchelewa kutekeleza majukumu yao
ya kazi na kuwapa usumbufu hasa kukitokea dharura nyakati za usiku.
Mkuu
wa kituo cha polisi Mlandizi,mrakibu Silvester Njau alieleza tatizo
hilo,wakati alipokuwa akipokea msaada wa mifuko ya saruji na matofali
kutoka katika umoja wa madereva wa Mlandizi-Dar es salaam ili kusaidia
ujenzi ulioanzishwa wa nyumba mbili za polisi.
Alisema
changamoto hiyo ni kubwa ambayo imemsukuma kuanzisha ujenzi huo ambapo
utakapokamilika utawezesha kuishi familia tatu hadi sita .
“Kwasasa
askari wote tunaishi uraia ambako ni mbali ikiwemo
Chalinze,Kibaha,Mbezi,Kiluvya ,Kibamba hivyo kutuweka katika wakati
mgumu na mazingira ya kazi”
“Ukimwita askari may be usiku
inakuwa ni ngumu sana kufika ukizingatia usafiri wa public nyakati za
usiku mwingi unakua haupo hivyo ni changamoto kubwa”alisema mrakibu
Njau.
Alieleza
kuwa wanaanza na ujenzi wa nyumba hizo mbili na baadae wataendelea na
zoezi hilo ili kuhakikisha kero ya kukosa makazi ya karibu unabaki
historia.
Mrakibu Njau ,alisema kila mmoja
anajukumu la kulinda nchi hivyo anaomba wadau wa amani wajitokeze
kuchangia kwa ari na mali ili kuondokana na kero ya ukosefu wa nyumba
kwa askari.
Alikishukuru
chama cha mapinduzi (CCM)Kibaha Vijijini kwa ushirikiano wake wa
kuhamasisha wadau na makundi mbalimbali ambapo wameweza kuzungumza na
umoja wa madereva ambao wamejitokeza kusaidia.
Akikabidhi
msaada huo,mwenyekiti wa madereva wa Mlandizi-Dar es salaam,Richard
Milinga,alisema wanatambua umuhimu wa polisi na amani hivyo wameguswa
kuchangia mifuko 10 ya saruji na matofali 400 vyenye thamani ya
sh.250,000.
Alisema
wanaendelea kujichangisha na baadae wanatarajia kutoa mifuko mingine 25
ya saruji ili kupunguza kero hiyo inayowakabili askari.
Awali katibu wa CCM ,Kibaha
Vijijini ,Enerst Makunga ,alisema mrakibu huyo aliwaeleza juu ya kuanza
kwa ujenzi huo na kutokana na umuhimu wa jambo hilo wameamua kuhamasisha
wadau wa maendeleo.
Alisema makazi hayo yatakapokamilika polisi watafanya kazi kwa tija kulinda jamii,usalama na amani iliyopo.
Makunga
alisema umoja wa madereva Mlandizi wamechangia kwa moyo sio kama wana
hela nyingi hivyo ni jukumu la makundi na watu wengine kuunga mkono
jambo hilo.
‘Wafanyabiashara ,viongozi na mti yeyote anaeguswa ajitokeze,
kwa kutambua huwezi kufanya kazi ama kufanyabiashara zako kama huna amani na ulinzi wa uhakika”alisema Makunga.
kwa kutambua huwezi kufanya kazi ama kufanyabiashara zako kama huna amani na ulinzi wa uhakika”alisema Makunga.
Alieleza
chama cha mapinduzi kitaendelea kuwa bega kwa bega na jeshi la polisi
kwa lengo la kuhakikisha sekta ya ulinzi na usalama inaimarika na
hatimae kupambana na uhalifu Mlandizi na kulinda usalama wa watu na mali
zake


No comments:
Post a Comment