Mkazi wa eneo hilo, Lukia Khalid (aliye kaa), akiwa amekaa nje na vyombo vyake baada ya kubolewa nyumba yake.
Wananchi
wa Tegeta A Kata ya Goba wakiwa wamesimama chini ya mti Dar es Salaam
jana, baada ya nyumba zao kubomolewa na Kampuni ya Udalali ya Yono kwa
madai ya kuvamia eneo hilo. Hata hivyo wamekanusha kuvamia eneo hilo.
Zaidi ya nyumba 150 zilibomolewa. Wananchi hao leo wanaandamana kwenda
kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kupeleka malalamiko yao.
Askari polisi wakiwa eneo hilo kuimarisha ulinzi.
Watoto wakiangalia nyumba yao baada ya kubomolewa.
Mkazi wa eneo hilo akiwa kando ya nyumba yake iliyobomolewa.
Mkazi wa eneo hilo akiangalia nyumba yake baada ya kubomolewa.
Magodoro yakiwa yamefunikwa na paa la nyumba baada ya kubomolewa kwa nyumba hizo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Udalali ya Yono Aution Mart imebomoa nyumba zaidi ya 150 za wakazi
wa Tegeta A Kata ya Goba jijini Dar es Salaam kwa madai ya kujengwa eneo
ambalo sio lao huku Kaya zaidi ya 450 zikikosa makazi ya kuishi.
Hata hivyo ubomojai huo umepingwa na wananchi hao wakidai eneo hilo ni lao na wapo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Zoezi
la ubomoaji wa nyumba hizo lililofanyika Dar es Salaam jana, ulisimamiwa
na askari polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku
wakiwa katika magari yenye namba PT, 3475, 1986 na 3675 huko kukiwa na
askari hao zaidi ya 15.
Mmoja
wa wananchi hao, Macarios Turuka akizungumza na Jambo Leo eneo la tukio
alisema eneo hilo kwa kipindi kirefu lilikuwa halitumiki na lilikuwa ni
vichaka vya wahalifu kwani wanawake walikuwa wakibakwa na kutumiwa na
watu kwa uhalifu ndipo walipoingia na kujenga.
Aliongeza
kuwa baada ya kuanza ujenzi ndipo alipo ibuka Benjamini Mutabagwa na
kueleza kuwa ni lake ndipo walipofungua kesi mahakama ya Kimara ambapo
alishindwa kupeleka vielelezo vya umiliki wa eneo hilo.
Mwanasheria
anayewatetea wananchi hao, Moses Chunga alisema kitendo cha kubomoa
nyumba hizo ni kukiuka sheria za mahakama kwani kuna kesi ya msingi
namba 188/ 2016 waliyofungua mahakama kuu ya ardhi ambapo walitakiwa
tarehe 31 mwezi huu kwenda kuisikiliza lakini wanashangaa kuona nyumba
hizo zikibomolewa.
Alisema
wananchi hao wanajipanga kudai fidia ya uhalibifu huo na kuwa kabla ya
yote wanahitaji kumuona rais kuona wanapata haki yao.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela alisema kampuni
yake imevunja nyumba hizo kwa amri ya mahakama na polisi walikuwepo
kusimamia zoezi hilo.
“Mwenye
eneo hilo ambaye ni Kanisa la Winers alishinda kesi mwaka mmoja
uliopita na leo jana ulikuwa ni utekelezaji wa kuwaondoa wavamizi hao”
alisema Kevela.
Mkazi
wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamisi alisema kitendo
walichofanyiwa si cha uungwana hata kidogo kwani wao wapo katika eneo
kwa siku nyingi mpaka wamefikia hatua ya kujenga nyumba hizo hizo
mmiliki huyo alikuwa wapi kwa siku zote hizo.
“Kwa kweli hawa watu wanatufanya tusiipende serikali yetu tunaomuomba rais atusaidie katika jambo hili” alisema Hamisi.
Hamisi
alisema kesho leo wanatarajia kwenda kwa mkuu wa wilaya ya Ubungo
kupeleka kilio chao na kama akishindwa watakwenda kwa mkuu wa mkoa na
kama napo hawatapata ufumbuzi watakwenda kumuona waziri Lukuvi na Rais.
Hawa Musa alisema baada ya kuvunjiwa nyumba zao wapo katika wakati mgumu na hawajui wataisheje na watoto wao.
Alisema
wamepanga vitu vyao nje na mvua yote iliyonyesha jana imelowanisha
vyombo vyao yakiwemo magodoro na hawajui huyo mtu anayedai ni eneo lake
nyuma yake yupo nani.
Alisema nyumba yake iliyobomolewa ilikuwa inathamani ya sh. 700,000.
“Tangua
tufungue kesi mahakama ya Kimara hakuwahi kufika kama yupo kweli
kwanini anashindwa kuhudhuria mahakamani ” alihoji Musa.
Musa
aliongeza kuwa kabla ya kubomoa nyumba hizo walipaswa kutoa notsi lakini
wao hawajafanya hivyo wamefika saa mbili asubuhi na kuanza kubomoa bila
hata ya kuwa shirikisha vipongozi wa eneo hilo.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo Juma Abdallah amelalamikia jeshi la polisi kwa
kuchukua TV, king’amuzi na sh. 80,000 zilizokuwepo ndani kabla ya nyumba
yake kubomolewa.
“TV yangu na king’amuzi na sh.80,000 zimechukuliwa wakati wa zoezi hilo” alisema Abdallah.
Katika
hatua nyingine wananchi hao wamemtupia lawama Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Tegeta A kuwa amekuwa akiwakumbatia watu wanaodai kuwa eneo
hilo ni lao wakati anaelewa fika ukweli halisi wa eneo hilo.
Mwenyekiti
huyo Marko Vaginga alipopigiwa simu ili kuzungumzia suala hilo hakuwa
tayari kuzungumza chochote zaidi ya kumtaka mwandishi kwenda ofisini
kwake kwa mazungumzo zaidi.
“Nakuomba uje ofisini tuzungumze kwa leo sipo tayari kuzungumza chochote” alisema Vaginga na kukata simu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni alipopigiwa simu alisema
polisi walikuwa eneo hilo kwa ajili ya kusimamia amri ya mahakama.


No comments:
Post a Comment