KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 7, 2016

WAPENDA MISOSI TAMASHA LENU HILI HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhS9u6-4s_mBWDdU_KkBFqKzKGBnI3wvO5A4yScgjDiJKA2_mW44hnBLE_h9OXtbDoxxzERVqqgQmHyvnV0J4kKxCl0tkVZGOFCb-ETRbpsVjzME1svczQ2K4p7GyiaG-ymgGmN6N3Wr2GK/s1600/w.jpg
 Mratibu wa Tamasha hilo Bi. Zahara Michuzi  akielezea juu maandalizi ya  tamasha la vinywaji na vyakula  litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya EM & U Investiment imeandaa tamasha la Chakula na Vinywaji
litakalofanyika (Dar es Salaam Food & Drink Festival) Jumamosi Oktoba 8, 2016  katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Edward James amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake kwa kushirikisha wapikaji  wa vyakula vya asili ikiwa ni kufanya Watanzania kuvipenda vyakula hivyo.
James amesema kuwa watu wengi wanapenda kula vyakula vya asili lakini hawajui watavipata wapi hivyo tamasha hilo litafungua ukurasa mpya juu ya watu kuweza kupata chakula hicho na sehemu gani.
Amesema katika tamasha hilo kutakuwa na wapishi katika kila kabila kupata chakula chake cha asili katika mikoa yao hiyo itakuwa ni sehemu kuwajengea utamdauni wa kupenda chakula cha asili.

James amesema katika tamasha hilo wananchi pia watapata huduma ya kupima afyazao na magonjwa yote bure katika Tamasha hilo wasanii mbalimbali watatumbuza.

No comments:

Post a Comment