Na Masanja Mabula –Pemba
VIONGOZI wa vyama vya upinzani hapa nchini wametakiwa
kuacha kusema mabaya Serikali pekee , bali wajenge utamaduni ya kuisifu
na kuipongeza Serikali pale inapofanya jambo la maendeleo kwa wananchi
wake .
Naibu Katibu Mkuu wa UDP Zanzibar Juma Khamis Faki amesema kwamba uwepo wa vyama vya upinzani ni kuikosoa Serikali lakini pale inapofanya jambo la maendeleo ni wajibu wao pia kuipongeza.
Akizungumza
na wandishi wa habari Kisiwani Pemba , Juma alisema baadhi ya wanasiasa
wa upinzani wanashindwa kutambua dhana ya demokrasia kwani wamekuwa
wakiitumia kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwa wananchi .
Alisema
kitendo kinachofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani
kinawajenga wafuasi wao kuamini kwamba maendeleo ya kweli yanaweza
kuletwa na wao jambo ambalo wanalifanya kwa ajili ya kujitafutia
umaarufu .
Aidha
alieleza kuwa katika kipindi hichi cha uongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya saba pamoja na ile ya Jamhuri ya
Muungano ya awamu ya tano zimewafanyia mambo mengi wananchi , hivyo ni
jukumu la wanasiasa kupanda kwenye viriri na kuyachambua moja baada ya
jengine .
“Ni
vyema viongozi wa vyama vya upinzani tukajenga utamaduni wa kuyatumia
majukwaa ya kisiasa kuwaeleza wananchi ukweli na uhalisia ya mambo
yanayofanywa na Serikali zao , tuacheni kasumba na kukosoa kila kitu
hata kama ni cha maendeleo ”alisema .
Alizidi kusema “Serikali za CCM zilizopo madarakani kwa hivi sasa zimewafanyia mambo mengi wananchi ikiwemo barabara ,
afya, elimu , maji na nishati ya umeme lakini wapinzani hatuyasemi ,
tuwaambieni ukweli wananchi na tusijitafutie umaarufu wa kisiasa tu
palipo na ukweli lazima usemwe ”aliongeza.
Katika
hatua nyingine Naibu Katibu huyo aliwashauri Viongozi wa CCM kuanzia
Jimbo hadi Mkoa kuwahamasisha wajumbe wa baraza la wawakilishi kufanya
kazi katika majimbo hayo ili kuleta utofauti kati ya waliowatangulia .
Alisema
wananchi walikuwa na matumaini ya mabadiliko ya maendeleo ndani ya
majimbo yao mara baada ya uchaguzi , lakini baadhi ya viongozi hao
wameyahama majimbo na kuyatelekeza na kushindwa kutimiza ahadi
walizozitoa.


No comments:
Post a Comment