
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika
Louis Rene Peter Larose (hayupo Pichani), makao Makuu ya Benki hiyo
Jijini Washington DC, Marekani, kulia kwake ni Katibu Mkuu w Wizara ya
Fedha na Mipango, Doto James.
(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango)

Ujumbe
wa wataalamu wa Fedha, Sera na Uchumi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa
makini Mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika,
Louis Rene Peter Larose (hawapo Pichani), Makao Makuu ya Benki hiyo
Jijini Washington DC, Marekani, ambapo unafanyika Mkutano wa Mwaka wa
Benki hiyo ambayo Tanzania ni Mwanachama, wa kwanza kushoto ni Kamishna
wa Sera Augustine Ollal, Kamishna wa Bajeti John Cheyo na Kaimu Kamishna
wa Fedha za Nje Mamelta Mutagwaba.

Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisalimiana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika,
Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC,
Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo
ya Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa
inaiwezesha Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025

Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, wakishikana mikono kuonesha umoja na mshikamano mara baada ya
kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter
Larose, Jijini Washington DC nchini Marekani, ambako ujumbe huo
unahudhuria Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo.


No comments:
Post a Comment