
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la
Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja (kulia)
akizungumza na vijana wenye umri chini ya miaka 18 kuhusu namna kijana
anavyopaswa kujitambua na maambukizi ya virusi vya ukimwi leo katika
viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani
Simiyu.

Baadhi ya vijana wenye umri chini
ya miaka 18 wakifuatilia mada iliyokua ikitolewa na Baraza la Taifa la
Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba
kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.

Mjumbe kutoka Baraza la Taifa la
Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bibi. Happiness Malamala (kulia)
akitoa elimu ya namna ya kutumia kinga kuzuia maambukizi ya virusi vya
ukimwi kwa vijana waliotembelea banda la NACOPHA leo katika viwanja vya
Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.

Mwezeshaji kutoka Baraza la Taifa
la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bw. Hamidu Mkwinda (kulia)
akitoa elimu ya kujitambua na namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi
vya ukimwi wakati wa ziara ya wajumbe kutoka NACOPHA walipotembelea
katika kituo cha mabasi cha Somanga leo
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Vijana nchini wametakiwa
kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili waweze kujitambua na kupata
mbinu mbadala zitakazowazesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya
ukimwi ili kujenga taifa lililo na afya bora.
Hayo yamesemwa na Mwezeshaji
kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA)
Bw. Hamidu Mkwinda alipokua akizungumza na vijana waliojitokeza kupata
elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa
wiki ya vijana kitaifa na kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru leo katika
Viwanja vya Sabasaba Mkoani Simiyu.
“Vijana wanatakiwa kujitambua na
kujua haki zao ili wasije wakaangukia katika wimbi la ulaghai na anasa
ambazo zitawapelekea kutokufikia malengo yao na wakati mwingine kupata
maambukizi ya virusi vya ukimwi bila kutarajia” amesema Bw. Mkwinda.
Aidha Bibi. Happiness Malamala
kutoka NACOPHA amewataka vijana kutokukata tamaa pale wanapojitambua
kuwa wamepata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani kuwa na virusi vya
ukimwi sio mwisho wa maisha bali watambue kwamba virusi vya ukimwi ni
kama magonjwa mengine yasiyotibika kama vile kisukari, kansa na presha.
Naye Mratibu kutoka Baraza la
Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja
amesema kuwa NACOPHA inashiriki katika Wiki ya Vijana kuelekea kilele
cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhakikisha vijana wanajua haki zao za
msingi hususani vijana wa kike waliopata jukumu la kuwa wazazi katika
umri mdogo wajue aina ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kukabiliana
nao.
Bw. Muhoja amesema kuwa NACOPHA
imejipanga kutoa amasa kwa vijana kuhusu ushauri nasaha na kupima ili
wajue hali yao ya kiafya na jinsi ya kujikinga na kuwakinga wengine,
lakini pia kupitia maonesho haya vijana wanapata elimu ya afya ya uzazi
na makuzi ili vijana waweze kujikinga na mimba zisizotarajiwa au kupata
watoto katika wakati usio sahihi.
NACOPHA kupitia ufadhili wa watu
wa Marekani (USAID) inatekeleza mradi wa SAUTI YETU, mradi unaojihusisha
na masuala ya ufuatiliaji, utendaji wa serikali na masuala ya utawala
bora, na pia kuwajengea uwezo wananchi waishio na VVU na UKIMWI ili
sauti zao zisikike, waweze kushirikishwa katika mambo ya maendeleo,
ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kutambua haki za msingi, kisheria
na kuchangia mawazo katika utekelezaji wa sera na sheria mbalimbali.
katika Mkoa wa Simiyu kuelekea
kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.


No comments:
Post a Comment