Zaidi
ya wakazi 5,000/=wa vijiji sita vya vya kata ya Mohoro ,Wilayani
Rufiji mkoani Pwani wamenufaika na mradi
wa elimu kuhusu afya ya uzazi na mtoto iliyotolewa kwa kipindi cha
mwaka mmoja na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana
naTaasisi ya uzazi na malezi bora (UMATI).
Takwimu hizo zilitolewa jana na Razia Mamboleo Ofisa wa Programu wa mradi huo Wilayani hapa ambao umehusisha vijiji vya Shela,Mohoro Mashariki,Mohoro Magharibi,Ndundutawa,King'ong' o pamoja na Kwaijia.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na changamoto za mradi huo Radhia alisema mradi huo umeleta mafanikio makubwa ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto,akina mama kupata mwamko wa kuhudhuria Kliniki kwa wakati mwafaka kipindi cha ujauzito sambamba na kuboreshwa kwa huduma za uzazi katika vijiji hivyo.
Aidha Radhia alibainisha kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia mradi huo umefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi sambamba na kuwapatia wanawake chanjo kwa wakati tofauti na awali .
Alijinasibu kuwa mradi huo umefanikiwa kutoa elimu kwa watoa huduma jumuishi (WAJA) ambao walipatiwa mafunzo kwaajili ya kuelimisha jamii jambo ambalo limeongeza uelewa wa masuala ya afya ya mama na mtoto katika jamii ya watu wa Rufiji.
Akizungumzia kuhusu changamoto za mradi huo ambao unafikia tamati Oktoba mwaka huu, Razia alieleza kuwa kikwazo kukibwa ni ya kieneo na kijiografia ambayo ufikaji wake ni wa kusua sua.
"Changamoto kubwa ni ya kieneo, maeneo mengine hayafikiki kutokana na miundo mbinu mibovu ambayo imesababisha magari kutofika"alisisitiza Razia.
Kwa upande wake mmoja wa Watoa elimu jumuishi (WAJA) Jumanne Mbondele alisema mradi huo umepata mwitikio chanya kwa wakazi wa Kata hiyo lakini changamoto kubwa ni ya kijiografia.
"Mwitikio ni mzuri sana na imesaidia sana Kuimaraisha afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo lakini mradi ni wa muda mfupi na ndiyo kama hivyo uanelekea ukingoni,tuanaomba mradi uongezewe muda angalau uwe wa miaka mitatau ili uweze kufikia maeneo mengine"alihitimisha Mbondele.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza alisema kuwa mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, afya ya mama na mtoto sambamba na matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanaume na wanawake.
"Vodacom
Tanzania Foundation itaendelea kusaidia jamii hasa katika masuala
mazima ya afya ili kutimiza malengo
ya milenia kuhakikisha sera ya afya ya kupunguza vifo vya mama na mtoto
sambamba na uboreshwaji wa afya ya uzazi "alihitimisha Rwehikiza. Takwimu hizo zilitolewa jana na Razia Mamboleo Ofisa wa Programu wa mradi huo Wilayani hapa ambao umehusisha vijiji vya Shela,Mohoro Mashariki,Mohoro Magharibi,Ndundutawa,King'ong'
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na changamoto za mradi huo Radhia alisema mradi huo umeleta mafanikio makubwa ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto,akina mama kupata mwamko wa kuhudhuria Kliniki kwa wakati mwafaka kipindi cha ujauzito sambamba na kuboreshwa kwa huduma za uzazi katika vijiji hivyo.
Aidha Radhia alibainisha kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia mradi huo umefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi sambamba na kuwapatia wanawake chanjo kwa wakati tofauti na awali .
Alijinasibu kuwa mradi huo umefanikiwa kutoa elimu kwa watoa huduma jumuishi (WAJA) ambao walipatiwa mafunzo kwaajili ya kuelimisha jamii jambo ambalo limeongeza uelewa wa masuala ya afya ya mama na mtoto katika jamii ya watu wa Rufiji.
Akizungumzia kuhusu changamoto za mradi huo ambao unafikia tamati Oktoba mwaka huu, Razia alieleza kuwa kikwazo kukibwa ni ya kieneo na kijiografia ambayo ufikaji wake ni wa kusua sua.
"Changamoto kubwa ni ya kieneo, maeneo mengine hayafikiki kutokana na miundo mbinu mibovu ambayo imesababisha magari kutofika"alisisitiza Razia.
Kwa upande wake mmoja wa Watoa elimu jumuishi (WAJA) Jumanne Mbondele alisema mradi huo umepata mwitikio chanya kwa wakazi wa Kata hiyo lakini changamoto kubwa ni ya kijiografia.
"Mwitikio ni mzuri sana na imesaidia sana Kuimaraisha afya ya mama na mtoto ikiwemo kupunguza vifo lakini mradi ni wa muda mfupi na ndiyo kama hivyo uanelekea ukingoni,tuanaomba mradi uongezewe muda angalau uwe wa miaka mitatau ili uweze kufikia maeneo mengine"alihitimisha Mbondele.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza alisema kuwa mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, afya ya mama na mtoto sambamba na matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanaume na wanawake.

No comments:
Post a Comment