![]() |
Kituo cha runinga cha Sound City (Sound City Tv) kimetoa orodha ya
wasanii na vipingele watakavyowani katika tuzo za Sound City MVP.
Kwa
upande wa Tanzania, katika tuzo hizo tutawakilishwa na Diamond
Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo.
Diamond yeye anawania tuzo
ya Msanii Bora wa Afrika (Best African Of The Year) na Msanii Bora wa
Kiume (Best Male), Ali Kiba atawania tuzo ya Video Bora ya Mwaka (Video
Of The Year) ambayo ni video ya wimbo wa aje, Vanessa Mdee yeye akitupa
karata yake katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike (Best Female) huku
Navy Kenzo wao wakichuana kwenye Kundi Bora la Muziki (Best Group).
|
November 28, 2016
DIAMOND, KIBA MDEE KUWANIA TUZO NIGERIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment