
Naibu waziri ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo akiagana na wanafunzi wa shule ya sekondari
msalato mara baada ya kuzungumza nao.
Wanafunzi wa kidato cha nne
wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo mara
baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika
Leo.
…………………………………………………………….
Naibu waziri Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo,
amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi
kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.
Katika ziara yake
kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo
amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya
udanganyifu.
Akizungumza na walimu
na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo
hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani
wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni
ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.
Ameeleza hatarajii
mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu kufanya
udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.
Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.
Akizungumza na
wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa
vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.
Hata hivyo
amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga
kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka
kuwajibika ipasavyo.


No comments:
Post a Comment