![]() |
Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba (katikati) akiungana na washikndi wa M-bet, Emmanuel Katema (kushoto) na Ramon
Mane,
kushangilia mara baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi wa Sh. Milioni
Arobaini na Sita kwa wahindi hao walioibuka kidedea wa Perfect 12.
Makabidhiano hayo byalifanyika jijini
Dar es Salaam leo Novemba 30, 2016.
Emmanuel Cornel Matema mwenye umri wa miaka 38 wa Tabata,
jijini Dar es Salaam na Mkazi wa Tabora, Ramon Hamisi Mane (22) wamefanikiwa kujishindia kila mmoja kiasi cha Sh milioni 23
baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi mbalimbali za ligi za Ulaya kupitia Kampuni ya m-Bet.
Washindi
wote hao, wamekabidhiwa vitita vyao katika hafla fupi iliyofanyika
ofisi za m-Bet, jijini Dar es Salaam Jumatano (Novemba
30, 2016) chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Tarimba aliwapongeza washindi hao na kuwataka
kuhakikisha wanazitumia vema fedha hizo ili ziweze kusawasaidia
katika kuboresha maisha yao.
“Nichukue
fursa hii kuwapongeza m-Bet kwa kuendesha bahati nasibu hii ambayo
imeonekana kuwanufaisha Watanzania wengi waliojishindia
mamilioni ya shilingi hadi sasa. Lakini pia nitoe rai kwa washindi
kuhakikisha wanazitumia ipasavypo fedha wanazoshinda ili ziweze
kuboresha maisha yao na si vinginevyo, ukizingatia kwa sasa maisha ni
magumu sana,” alisema Tarimba.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi
wa m-Bet, Dhiresh Kabba, alisema kuwa wawili hao walifanikiwa kuzoa
kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 15 za ligi za
Ulaya.
“Tunafarijika kuwakabidhi
Matema na
Mane kitita chao kiasi cha Sh milioni 23 ambapo watagawana sawa sawa,” alisema Kabba.
Aliwataka
watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki
halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu
kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote unaondoka na
kitita chako mchana kweupe.
Akielezea furaha yake kwa kushinda fedha hizo,
Matema
ambaye ni mjasiriamjali, alisema: “Nawashukuru sana m-Bet kwa
kuniwezesha kushinda fedha hizi ambazo nitazitumia kuongeza mtaji wa
biashara zangu na mahitaji binafsi.”
Naye
Mane
ambaye ni mwanafunzi na mjasiriamali, alisema: “Fedha hizi zitanisaidia
sana katika biashara zangu, lakini zaidi ikiwa ni masomo kwani nimekuwa
katika wakati mgumu linapokuja
suala la ada na mahitaji mengineyo ya shule. Ahsante sana m-Bet.”
Kuhusu
m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa
leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya
upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha
(Sim Betting) nchi nzima
“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Perfect 12 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-Bet,” alisema Kaba. |
November 30, 2016
WAKAZI WA TABATA, ARUSHA WALAMBA MIL.46 ZA M-BET
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment