KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 1, 2016

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI NA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA)

gofu__george_wasira
Kufuatia Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Jenerali (Mst) George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA tarehe 29 Oktoba, 2016, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Profesa Jumanne A. Maghembe (Mb) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Uanzishwaji wa TANAPA Sura ya 282 Jedwali la Pili ikisomwa pamoja na kifungu cha 8(1)(b) cha Sheria hiyo.
  1. Bi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania.
  2. Dkt. Lucy Lugwisha, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi  
wa Mazingira.
  1. Kamishina Marijan M. Sato, Mkuu wa Operesheni  na Mafunzo,    Makao Makuu  Jeshi la Polisi.
  2. Profesa Alexander Songorwa, Mkurugenzi wa Wanyamapori     kutoka   Wizara ya Maliasili na Utalii.
  3. Profesa Wineaster Anderson, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar  es  Salaam, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii Endelevu Afrika (NARESTi Africa).
  4. Bw. George Fumbuka, Mhasibu aliyethibitishwa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya CORE Securities.
  5. Dkt. Chanasa Mpelumbe Ngeleja, Daktari Mkuu wa Mifugo,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
  6. Bw. Allan J. H. Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.  
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 29/10/2016 hadi tarehe 28/10/2019.
    IMETOLEWA NA
Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi
KATIBU MKUU
WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII
30 Novemba, 2016

No comments:

Post a Comment